• Call us: +255 755 446 540
  • Email: info@tecden.or.tz
Tanzania Early Childhood Development Network (TECDEN)
SUPPORT US
  • Home
  • Who We Are
    • Overview
    • Constitution
    • Vision and Mission
    • Strategic Plans
    • Our Partners
    • Our Team
  • Our Work
  • Members
  • News & Resources
    • News and Events
    • Conferences
    • Reports and Publications
    • success stories
    • Photo Gallery
    • Video Gallery
  • Contact Us

Ufahamu Mtandao wa Malezi Makuzi na Maendeleo ya Watoto Wadogo Tanzania (TECDEN)

  /   News and Resources   /   Ufahamu Mtandao wa Malezi Makuzi na Maendeleo ya Watoto Wadogo Tanzania (TECDEN)
Jan 19, 2015
Ufahamu Mtandao wa Malezi Makuzi na Maendeleo ya Watoto Wadogo Tanzania (TECDEN)
19Jan

Mtandao wa Malezi Makuzi na Maendeleo ya Watoto Wadogo Tanzania – TECDEN ni chombo kinachoundwa na mashirikia mbalimbali yanayofanya kazi za kuhudumia watoto wadogo Tanzania. 

Mtandao huu ulianzishwa mwaka 2000 na kusajiliwa rasmi mwaka 2004. Makao makuu ya Mtandao huu yapo Jijini Dar es salaam. 

Hadi kufikia mwaka 2014 Mtandao huu una jumla ya mashirika wanachama wasiopungua 200 katika mikoa 14 ya Tanzania bara na Visiwani yanayotoa huduma kwa watoto wadogo Tanzania Lengo kuu la Mtandao ni kuboresha huduma za watoto wadogo Tanzania ili waweze kukua na kufikia utimilifu wao Shughuli Kuu za Mtandao ni pamoja na:- • Kufanya ushawishi na utetezi wa masuala yanayohusu uboreshaji wa huduma na kulinda haki za watoto wadogo ikiwa ni pamoja na kushawishi maboresho ya sera na kufuatilia utekelezaji wa sheria na miongozo mbalimbali inayohusu uboreshaji wa huduma kwa watoto wadogo Tanzania. • Kuhamasisha jamii na watoa huduma kutambua umuhimu wa kuimarisha na kuwezesha watoto wadogo kupata mahitaji na haki zao za msingi. • Kuimarisha mifumo ya upashanaji habari na kuelimishana katika ngazi zote za huduma kwa watoto wadogo. • Kutafiti na kutumia matokeo ya utafiti katika kushauri uboreshaji wa huduma kwa watoto wadogo Tanzania.

Dhana ya Malezi Makuzi na Mendeleo ya Awali ya Mtoto (MMMAM) Malezi, makuzi na maendeleo ya awali ya mtoto ni istilahi ya jumla ya programu na vitendo vinavyoandaliwa kuwasaidia watoto (kuanzia mimba, kuzaliwa hadi miaka 8) ili kukua vizuri kimwili, kiakili, kijamii, kihisia, kimaadili na kiroho.

Watoto wanahitaji kuchangamshwa katika nyaja na hatua zote za ukuaji, kiakili kwa michezo, kujifunza kuzungumza, kukaa, kutambaa, kutembea na kupatiwa fursa ya kuanza kujifunza mambo mbalimbali pamoja na utamaduni wao.

Utoaji wa huduma jumui za MMMAM. Huduma hizi hujumuishwa ili kuwawezesha watoto wengi kupata huduma jumuishi za MMMAM zitolewazo na sekta mbali mbali katika mkabala jumui. Huduma hizi zinapaswa kupatikana kuanzia ngazi ya familia ,vituo vya afya ya msingi,vituo vya kulelea watoto mchana, vituo vya Malezi Makuzi ya awali ya mtoto vinavyomilikiwa na Jamii, madarasa ya awali na madarasa ya msingi hususani darasa la kwanza na la pili.

Katika kutekeleza shughuli zake Mtandao wa TECDEN umekuwa ukishirikiana na mashirika mbalimbali ya wabia wa maendeleo ikiwemo shirika la Children in Crossfire kutoka nchini Ireland na shirika la Better Way Foundation kutoka nchini Marekani.

Ili kujua habari zaidi za TECDEN na masuala ya utoaji huduma kwa watoto wadogo na faida zake, unaweza kutembelea ofisi ya Mtandao makao makuu iliyopo Jengo la Posta mkabala na Wizara ya Mambo ya Ndani Nchi na Makao Makao Makuu ya Polisi jijini Dar es Salaam.

Unaweza pia kuwasiliana kwa njia ya simu au barua pepe na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Ndugu Bruno Ghumpi kwa namba 0754 690 556 na barua pepe ecdnetwork@gmail.com na ghumpibr@yahoo.com

Categories

  • News and Events41
  • Conferences4
  • Reports and Publications11
  • success stories 2

Other Posts

  • Sep 06, 25 Call for Consultancy on Assessment of ECD Public Expenditure Review in the Implementation of NM-ECDP I (2021/2022-2025/2026)
  • Aug 25, 25 CALL FOR APPLICATION FOR   CIVIL SOCIETY ORGANIZATIONS TO SUPPORT THE ESTABLISHEMENT OF COMMUNITY ECD CENTRES ACROSS 15 REGIONS OF TANZANIA MAINLAND
  • Jul 23, 25 Tanzania Early Childhood Development Network’s (TECDEN) participation in the Kenya’s 6th National ECD Stakeholders’ Conference. 
  • Jul 21, 25 Tanzania Vision 2050: Placing Early Childhood Development at the Heart of National Transformation
  • Jun 17, 25 COMMEMORATION OF THE DAY OF THE AFICAN CHIL (DAC) 2025

Facebook

Tanzania Early Childhood Development Network (TECDEN)

Our Address

  • Area D-Mlimwa East Plot Number 30 Block K, Dodoma,
  • info@tecden.or.tz
  • +255 755 446 540
  • +255 755 446 540

Quick Links

  • Who We Are
  • What We Do
  • Our Team
  • Our Members
  • Our Partners
  • News & Events
  • Publications
  • Photo Gallery
  • Video Gallery
  • Contact Us
  • Our Locations
  • Privacy Policy

Follow Us

+255 755 446 540

By subscribing to our mailing list you will get the latest news from us.

REQUEST WITH ONLINE FORM

Whats New

  • Call for Consultancy on Assessment of ECD Public Expenditure Review in the Implementation of NM-ECDP I (2021/2022-2025/2026)
  • CALL FOR APPLICATION FOR   CIVIL SOCIETY ORGANIZATIONS TO SUPPORT THE ESTABLISHEMENT OF COMMUNITY ECD CENTRES ACROSS 15 REGIONS OF TANZANIA MAINLAND
  • Tanzania Early Childhood Development Network’s (TECDEN) participation in the Kenya’s 6th National ECD Stakeholders’ Conference. 
  • Tanzania Vision 2050: Placing Early Childhood Development at the Heart of National Transformation
  • COMMEMORATION OF THE DAY OF THE AFICAN CHIL (DAC) 2025
Copyright © 2025 - Tanzania Early Childhood Development Network (TECDEN)