Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Nurdin Babu ametoa wito kwa Viongozi wa Halmashauri za Wilaya za Mkoa wa Kilimanjaro kuweza kusimamia kikamilifu utekelezaji wa programu ya Malezi ,Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto( PJT -MMMAM) kwa kufanya uzinduzi ngazi za Wilaya na kutenga bajeti itakayowezesha utekelezaji wa program hiyo.
Mhe. Babu ameyasema hayo Julai 26, 2023 wakati wa uzinduzi wa programu jumuishi ya taifa ya malezi ,makuzi na maendeleo ya awali ya mtoto PJT_MMMAM katika ukumbi wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa.
Hata hivyo,Mhe Babu amewataka wazazi na walezi kutenga muda wa kukaa, kucheza na kuzungumza na watoto ili kuwajenga watoto kiakili, kihisia,kimwili na kimaadili.
Aidha, amewataka Wadau wa Mashirika yasiyo ya kiserikali na Wasimamizi wa vituo vya kulelea watoto mchana(ECDs) waweze kufanya ufuatiliaji wa vituo vyote na madarasa ya awali ili kuweza kujiridhisha na uendeshaji wa vituo hivyo.
https://www.instagram.com/p/CvMW-rKOqk5/?utm_source=ig_web_copy_link&igshid=MzRlODBiNWFlZA==